Sports and Entertainment

Jumatano, 15 Oktoba 2014

TANZIA : PROF. MAZRUI AAGA DUNIA

Hakuna maoni :

Msomi maarufu wa Kenya Profesa Ali Alamin Mazrui amefariki dunia leo asubuhi jijini New York, Marekani akiwa na umri wa miaka 81.
Mazrui alikuwa profesa katika chuo kikuu cha Binghamton jijini New York.
Ameandika vitabu 30 ambavyo vimezungumzia masuala ya uongozi na siasa za Afrika na Kimataifa pamoja na masomo ya kiislamu. Je, unamkumbuka vipi msomi huyo?
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Aamin.
Chanzo: DW Kiswahili.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni