Sports and Entertainment

Jumatano, 29 Oktoba 2014

Tigo na Facebook kushirikiana zaidi

Hakuna maoni :

Kampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania ya Tigo, leo imezindua ushirikiano mpya na Facebook kuanzisha huduma mpya ijulikanayo kama internet.org ambayo itawezesha wateja wote wa Tigo kuipata bure.
Shughuli hiyo imefanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar Es Salaam.
Mwakilishi wa Tigo, David Zachakaria amewaeleza waandishi wa habari kuwa mpango huo unalenga kuwapa wateja huduma mpya na za kisasa kwa wakati unaostahili.
Vile vile mwakilishi wa Facebook, Naheed Hirji amesema internet.otg ilianzishwa mwaka jana kwa lengo la kutoa fursa sawa kwa mamilioni ya watu hata katika nchi ambazo hazikuwa na mitandao iliyopiga hatua.
Ametaja kuwa mradi huo unashirikisha makampuni mbali mbali ya simu za mkononi ambayo yatasaidia kuufikisha mradi huo kwa watu wengi zaidi.
Kutakuwa na taarifa za habari za ajira, afya, kiuchumi, habari za kimataifa na nyinginezo.
Wateja watakaotaka kuitumia wanatakiwa kupakua app ijulikanayo kama internet.org kutoka Play Store.
Maelezo zaidi yatafuata.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni