Jumanne, 28 Oktoba 2014
wanaowania mchezaji bora wa Dunia

Mchezaji mwenza wa Bale Real Madrid, Cristiano Ronaldo alishinda tuzo ya pili ya Ballon d’Or mjini Zurich mwaka uliopita.
Nyota watano wa Ligi Kuu ya Uingereza na Muingereza mmoja Gareth Bale – wametajwa kwenye orodha ya majina 23 kwa ajili ya tuzo ya Ballon d’Or.
Mshikiliaji wa tuzo hiyo kwa sasa Cristiano Ronaldo na mshindi mara nne Lionel Messi wapo tena ila hakuna nafasi kwa mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Luis Suarez, ambaye alifungiwa kwa miezi minne mwezi Julai kwa kumng’ata Giorgio Chiellini wa Italia kwenye Kombe la Dunia.
Wachezaji sita wa Ujerumani waliocheza Kombe la Dunia wametajwa, na kukifanya iwe nchi yenye wawakilishi wengi kwenye orodha hiyo.
Wachezaji watano walioko Uingereza ambao wametajwa kwenye orodha hiyo ni wana-Chelsea watatu ambao ni Eden Hazard, Diego Costa, Thibaut Courtois, Manchester City ni Yaya Toure na Angel Di Maria wa Manchester United.

Wachezaji sita wa mabingwa wa Kombe la Dunia Ujerumani wametajwa kuwania tuzo hiyo akiwemo nahodha Philipp Lahm (wa pili kushoto).
ORODHA YA WACHEZAJI 23 WANAOWANIA BALLON d’Or
Gareth Bale (Wales), Karim Benzema (France), Diego Costa (Spain), Thibaut Courtois (Belgium), Cristiano Ronaldo (Portugal), Angel Di Maria (Argentina), Mario Gotze (Germany), Eden Hazard (Belgium), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), Andres Iniesta (Spain), Toni Kroos (Germany),
Wengine ni; Philipp Lahm (Germany), Javier Mascherano (Argentina), Lionel Messi (Argentina), Thomas Muller (Germany), Manuel Neuer (Germany), Neymar (Brazil), Paul Pogba (France), Sergio Ramos (Spain), Arjen Robben (Holland, James Rodriguez (Colombia), Bastian Schweinsteiger (Germany), Yaya Toure (Ivory Coast).
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni