Jumatano, 29 Oktoba 2014
Zambia kuongozwa na mzungu baada ya Raisi wake kufariki
Makamu wa Rais wa Zambia, Guy Scott, ametajwa kuwa kiongozi wa muda kutokana na kifo cha Rais Michael Sata kilichotokea jana nchini Uingereza.
Uchaguzi wa kumpata Rais wa kudumu utafanyika ndani ya siku 90, alisema Waziri wa Ulinzi Edgar Lungu, habari hizi ni kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC.
Bw Scott anakuwa rais wa kwanza mweupe au mzungu kuongoza taifa la Afrika tangu alipoondoka FW de Klerk aliyeongoza Afrika Kusini wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi.
Bw Sata alikufa akiwa na umri wa miaka 77 wakati akitibiwa maradhi ambayo mapaka sasa hayajatwa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni