Bonanza

Sports and Entertainment

Alhamisi, 29 Januari 2015

Obama azua gumzo Saud Arabia

Hakuna maoni :

Michelle Obama wakati wa Ziara ya Rais Obama Saudi Arabia 
 
Mkewe Rais wa Marekani Barack Obama, Michelle Obama alipowasili nchini Saudi Arabia na mumewe bila ya kujitanda kichwa chake kwa kitambaa, wengi walitarajia kwamba mitandao ya kijamii nchini humo ingewaka moto kwa mingon'ono.

Lakini mambo yalikuwa tofauti maana kimya kilikuwa kikuu. 

Ingawa vyombo kadhaa vya habari Ulaya, viliripoti kuhusu utata mkubwa kutokea kwenye mitandao ya kijamii, alama ya njia ya reli kwenye mtandao wa Twitter kwa lugha ya kiarabu...ikimaanisha ....''Michelle Obama bila mtandio''...ujumbe huo ilisambazwa kwenye mtandao huo zaidi ya mara 2,5000.

Hii sio idadi kubwa ya watu waliousambaza ujumbe huo lakini pia sio ndogo sana katika nchi yenye watumiaji wengi wa Twitter.

Pia inaarifiwa ujumbe huo ulizidiwa nguvu na ujumbe mwingine uliotumwa kwenye Twitter dhidi ya ziara ya Rais Obama nkatika ufalme huo.

''Mfalme Salman amwacha Obama na kwenda kuomba,'' huu ndio ulikuwa ujumbe mwingine uliosambazwa sana kwenye Twitter kuhusu ziara ya Obama nchini humo.
Ujumbe huo: "Mfalme Salman amwacha Obama na kwenda kuomba,'' uliwavutia zaidi ya watu 170,000.
Kuna baadhi ya viongozi waliowahi kwnda Saudia bila ya kufunika vichwa vyao
Wananchi katika ufalme huo walisambaza ujumbe huo kama njia yao ya kuonyesha wlaivyofurahishwa na mfalme mpya, Salman kumwacha Obama na kwenda kusali,kama ilivyoonekana kwenye video iliyowekwa kwenye Youtube.

''Huyu ndiye mwanamume aliyemwacha kiongozi wa nchi muhimu zaidi duniani akimsubiri wakati akienda kusali'', aliandika mtu mmoja kwenye mtandao wa Twitter.

Jumanne, 13 Januari 2015

Ronaldo wins Ballon d'or

Hakuna maoni :
Cristiano Ronaldo wins Fifa Ballon d'Or
Real Madrid attacker Cristiano Ronaldo has won the 2014 Fifa Ballon d'Or ahead of Bayern Munichgoalkeeper Manuel Neuer and Barcelona forward Lionel Messi, scooping up the prestigious individual award for the third time in his career.

Ronaldo enjoyed a hugely successful 2014, in which he guided Madrid to Champions League glory by netting a record 17 goals in one campaign, and earned 37.66 per cent of the votes.

Additionally, the prolific attacker played an integral part in the Santiago Bernabeu side's Copa del Rey win by netting three goals in six appearances, even if he missed the final against Barcelona due to injury.

On an individual level, the 29-year-old won the Liga top scorer award by scoring 31 goals in 30 appearances, which also saw him crowned joint-winner of the European Golden Shoe together with Luis Suarez.

Ronaldo becomes the seventh player in history to successfully defend his Ballon d'Or title after Johan Cruyff, Kevin Keegan, Karl-Heinz Rummenigge, Michel Platini, Marco van Basten and Messi.

The Portugal international was first voted the world's best in 2008, when he pipped Messi and Fernando Torres to the coveted trophy. He then had to settle for second spot in 2009, 2011 and 2012 before winning the award a second time in 2013, this time ahead of Messi and Franck Ribery.

The former Manchester United star has moved level with Cruyff, Platini and Van Basten on three wins, with only Messi ahead of him on four Ballon d'Or trophies.

"I want to thank my mother, my family. I would like to thank all those who voted for me, my coach, my fellow players, the president of the club," Ronaldo commented while collecting the award.

"It has been an unforgettable year. To win this trophy, a trophy of this kind, is something unique, and like I say, I want to continue working as I have so far, trying to go on and win more titles both individually and as a team, for my mother, for my father who is up there looking at me, my son, and to become better. 

"I would like to say to the Portuguese: I never thought I would win this trophy on three separate occasions. Of course it is something that is always with me - I want to become one of the greatest players of all time and I hope to get there. I want to thank you all," concluded the Madrid star before leaving the stage with a loud roar.

Messi, meanwhile, made it to the podium for the seventh time in succession after he was crowned all-time top goalscorer of La Liga and the Champions League in 2014, and amassed 15.76% of the final vote.

Neuer missed out on the chance to become the first goalkeeper to win the award since Lev Yashin in 1963 after guiding Germany to World Cup glory and winning the Bundesliga title and DFB-Pokal with Bayern. He earned 15.72% of the vote.

Alhamisi, 11 Desemba 2014

Dr.dre ndiye mwanamuziki alieingiza pesa nyingi kuliko wote Duniani

Hakuna maoni :
null

Baada ya kuongoza kwenye orodha ya ‘Forbes’
Hip-Hop Cash Kings’ miezi kadhaa iliyopita ,
producer mkongwe, rapper na mfanyabiashara Dr.
Dre ameongoza tena kwenye orodha nyingine ya
Forbes ya wanamuziki wanaolipwa zaidi ‘Forbes
World’s Highest Paid Musicians 2014’.
Dr. Dre amekamata nafasi hiyo kwa kutengeneza
$ 620 million mwaka huu, Kiasi ambacho
kimechangiwa zaidi na deal yake ya Beats By Dre
na Apple.
Amemzidi Beyonce aliyekamata nafasi ya pili kwa
kuingiza dola milioni 115 ambazo zimetokana na
ziara yake ya Mrs Carter World Tour, mauzo ya
album yake ya kushtukiza pamoja na
endorsements deals zikiwemo za Pepsi na H&M.
Jay Z yuko kwenye orodha hii lakini amefungana
na Diddy pamoja na Bruno Mars kwenye nafasi
ya 12 kwa kutengeneza $60 million.
Katika kutengeneza orodha hii Jarida la Forbes
limezingatia vitu vifuatavyo, mapato yatokanayo
na ziara za muziki, mauzo ya muziki, publishing,
endorsements, merchandise pamoja na biashara
nyingine zilizofanywa na wanamuziki katika
kipindi cha June 2013-June 2014.
Hii ni orodha kamili ya Forbes World’s Highest
Paid Musicians 2014:
1. Dr. Dre ($620 million)
2. Beyoncé ($115 million)
3. The Eagles ($100 million)
4. Bon Jovi ($82 million)
5. Bruce Springsteen ($81 million)
6. Justin Bieber ($80 million)
7. One Direction ($75 million)
8. Paul McCartney ($71 million)
9. Calvin Harris ($66 million)
10. Toby Keith ($65 million)
11. Taylor Swift ($64 million)
12. Jay Z ($60 million)(tie)
12. Diddy ($60 million)(tie)
12. Bruno Mars ($60 million)(tie)
15. Justin Timberlake ($57 million)
16. Pink ($52 million)
17. Michael Bublé ($51 million)
18. Rihanna ($48 million)
19. Rolling Stones ($47 million)
20. Roger Waters ($46 million)
21. Elton John ($45 million)
22. Kenny Chesney ($44 million)
23. Katy Perry ($40 million)
24. Jason Aldean ($37 million)(tie)
24. Jennifer Lopez ($37 million)(tie)
26. Miley Cyrus ($36 million)(tie)
26. Celine Dion ($36 million)(tie)
28. Muse ($34 million)(tie)
28. Luke Bryan ($34 million)(tie)
30. Lady Gaga ($33 million)(tie)
30. Drake ($33 million)(tie)

Jumamosi, 6 Desemba 2014

wanawake wasisitizwa kutofumbia macho rushwa ya n gono

Hakuna maoni :
Msanii wa kizazi kipya Meninah Abdulkareem akiwa nyumbani kwake


Mwanadada wa muziki wa kizazi kipya Meninah Abdulkareem ‘Meninah,’ amewatolea uvivu ‘maprodyuza’ wanaopenda rushwa ya ngono, akisema kwake hawatafanikiwa.
Amesema anakerwa na tabia hiyo na inaweza kumfanya msanii akate  tamaa ya kufanya muziki kwa ajili ya tabia hizo.
Akizungumza juzi, Menina alisema si jambo jema kwa maprodyuza kufanya hivyo kwa sababu inawavunja moyo wasanii wachanga.
“Nasikitishwa mno na hali kama hiyo kuendelea kwenye soko la muziki na kama huwezi kumsaidia binadamu mwenzako ni bora useme kuliko kutaka rushwa ya ngono.
Meninah aliendelea kusema kamwe, hawezi kukubaliana na hali hiyo na amewashauri  wasanii wengine wa kike kupambana vikali dhidi ya jambo hilo.
“Sitakubaliana na rushwa ya ngono na wasanii wa kike tunapaswa kutolifumbia macho jambo hili,” alisisitiza Menina.

Mchezaji afariki baada ya kupigwa kichwa

Hakuna maoni :
Mchezaji Franco Nieto aliyefariki baada ya kupiwa na jiwe kwenye kichwa wakati wa mechi nchini Argentina
Mchezaji wa Argentina Franco Nieto ,mwenye umri wa miaka 33 amefariki baada ya kupigwa kwenye kichwa wakati wa mechi siku ya jumamosi.
Nieto ,nahodha wa kilabu ya kijimbo ya Tiro federal alishambuliwa na genge baada ya mechi kati ya wapinzani wao wa jadi Chacarita Juniors katika mji wa Aimogasta kazkazini magharibi mwa Argentina.
Mechi hiyo ilisimamishwa kwa dakika 15 kabla ya kukamilika baada ya refa kuwapa kadi nyekundu wachezaji wanane kwa kupigana.
Mwaka huu watu 15 wamefariki katika ghasia zilizosababishwa na soka nchini Argentina,Binamu wa Nieto,Pablo Nieto amesema kuwa watu watatu walimzunguka mchezaji huyo alipokuwa akielekea katika gari lake na mkewe na mtoto wao wa mwezi mmoja.
Walimpiga kwa ngumi na mateke kabla ya mmoja ya watu hao kumpiga na jiwe katika kichwa na kumwacha bila fahamu.
Alifanyiwa upasuaji siku ya jumanne lakini akafariki siku ya jumatano.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Fabian Bordon ameviambia vyombo vya habari kwamba watu watatu wamekamatwa kutokana na shambulizi hilo.
Ghasia zinazosababishwa na soka ni tatizo kubwa nchini Argentina.
Kulingana na shirika moja lilisokuwa la kiserikali Salvemos el Futbol,vifo vinavyosababishwa na ghasia za soka vimeongezeka mwaka huu.
Washukiwa wakuu ni genge la Barras Bravas ambao hudhibiti maneo ya kukalia katika viwanja vya mpira na barabara karibu na viwanja hivyo.

Tata Martino ajutia msimu wake mbaya Barca

Hakuna maoni :
Martino: I regret everything I did at Barcelona

Kocha wa zamani wa magwiji wa soka la Hispania, Barcelona ; Tata Martino amedai kwamba anajutia msimu mbaya aliokumbana nao wakati yuko katika klabu hiyo, Martino mwenye miaka 52 amesema kuwa licha ya kufanya kwake hovyo lakini angepewa muda hadi sasa mambo yangekuwa shwari Catalan


"Kutokana na mawasiliano yetu ya kwanza,  ningefanya karibu kila kitu tofauti," aliiambia Marca.

 "Mimi sikutoa mifano yoyote, lakini mimi najuta mambo mengi yaliyotokea wakati huo, ingawa wameweza imenisaidia kujifunza na si kurudia makosa kama hayo."

Kocha huyo wa zama ni wa Paraguay alikwenda mbele zaidi na kumpigia chapuo Leo Messi katika tuzo ya mchezaji bora wa Dunia na kusisitiza kuwa shirikisho la soka Duniani lifikirie tena juu ya tuzo hizo

"Baadhi ya makocha hawaangalii sana juu ya suala hilo," alisema.

 "Mimi ni mmoja wao. Kama Messi ni katika anashindana, nataka ashinde. nitampigia kura yeye

Labda tunapaswa kufikiria upya juu ya nani anapiga kura kwa ajili ya tuzo hii. Kuna mambo mengi binafsi."

Hata hivyo Messi ambae hakushinda taji lolote msimu uliopita anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mshindi wa kombe la Dunia mlinda mlango Manuel Neuer pamoja na mtambo wa mabao wa  mabingwa wa Ulaya Real Madrid, Mreno Cristiano Ronaldo ambapo mshindi atatangazwa januari 12

Sserenkuma atua Simba

Hakuna maoni :

Mshambuliaji matata wa kilabu ya Gor Mahia nchini Kenya Dan Sserenkuma aihama kilabu hiyo na kujiunga na Simba SC ya Tanzania
Aliyekuwa Mshambuliiaji wa mabingwa wa soka nchini Kenya Gor Mahia Dan Serenkuma amejiunga na kilabu ya Tanzania Simba SC.
Raia huyo wa Uganda alijiunga na kilabu hiyo ya Ligi ya Vodacom na kutamatisha kazi yake ya miaka mitatu katika ligi ya Kenya ambapo alianza kwa kuichezea Nairobi City Stars kabla ya kujiunga na Gor ambapo alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa ligi mara mbili.
''Nimefurahia miaka miwili na nusu katika kilabu ya Gor Mahia,lakini huu ndio wakati muhimu wa kuaga.Tumefurahia nyakati maalum na mafanikio pamoja,na habiki wamenisaidia sana hususan wakati mgumu'',Mfungaji huyo wa mabao mengi katika ligi ya Kenya aliandika katika mtandao wake wa Twitter.
''Ningependa kumshukuru kila mtu katika usimamizi wa kilabu kwa kunipa fursa muhimu ili kuonyesha kipaji changu.
Dan Sserenkuma
Mchezaji huyo wa kimataifa katika timu ya Uganda Cranes alipigwa picha katika mtandao wa kilabu hiyo akifanyiwa majaribio pamoja na kupimwa afya na sasa anatarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake katika barabara ya Msimbazi mjini Daresalaam tayari kwa maandalizi ya mechi za ligi ya Tanzania.
Wakati huohuo imebainika kwamba Kilabu ya Gor Mahia ilishindwa kumzuia mchezaji huyo.
Duru zimearifu kuwa mchezaji huyo aliandamwa na kilabu ya Gor mahia kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba alitarajiwa kujiunga na Simba.
Lakini Gor Mahia haikuwasilisha ombi lolote la fedha kwa kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa ameweka kandarasi yenye thamani ya shilingi millioni 3 pamoja na mshahara wa ksh.250,000 kwa mwezi na kilabu hiyo ya Tanzania ambapo atajiunga na mchezaji mwengine wa Gor Mahia Mungai Kiongera.