Alhamisi, 26 Juni 2014
Balotelli afunga watu midomo mitandaoni, awapa makavu
Nyota mwenye utata Mario Balotelli amewajibu kwa kile kinachosemekana kuwa ni wabaguzi wa rangi baada ya kulaumiwa kwa Italia kutolewa kwenye Kombe la Dunia.
Video ya kwenye mtandao wa kijamii iliyotumwa kwenye mtandao wa Instagram na raia wa Italia iliandikwa hivi: “Mario, hivi unajua mambo yalivyo? Wewe sio Muitaliano, toka.”
Balotelli alijibu video kwa kutumia linki hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter.
“Mimi ni Mario Balotelli, nina miaka 23, sikuchagua kuwa Muitalia”, alisema.
“Nilitaka kuwa hivyo kwa sababu nilizaliwa Italia na daima nimeishi Italia.
Hili Kombe la Dunia lilikuwa na maana kubwa kwangu, nasikitika, nina hasira na nimefadhaika, mimi binafsi”.
“Msinitupie lawama mimi tu pekee kwa sasabu Mario Balotelli alijitolea kila kitu kwa ajili ya timu ya taifa na sikuharibu chochote, hivyo tafuteni sababu nyingine kwa sababu Mario Balotelli ana mawazo mapya sasa ya kusonga mbele kwa nguvu zote kuliko awali huku kichwa kikiwa juu”.
“Najivunia kuwa nimejitolea kila kitu kwa ajili ya nchi hii. Au labda, kama mnavyosema, mimi sio Muitalia. Waafrika wasingethubutu kumtupa mmoja wa ndugu wao, Kamwe.
“Kwa hilo tuheshimuni Waafrika, kama mnavyotuita, tuna nuru ya baadae. Aibu sio kukosa goli ama kukimbia kidogo au zaidi. Aibu ni kwa haya mambo. Kweli Waitalia! Kweli?.
Sio mara ya kwanza kwa Balotelli kukumbana na wafuasi wa ubaguzi wa rangi nchini Italia.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni