Jumatano, 25 Juni 2014
Congo wazima umeme kwa ajili ya kombe la Dunia
Homa ya Kombe la Dunia imeilazimu kampuni ya umeme ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwaomba wateja wake kuzima kila kitu kasoro runinga (tv), ili kuwe na umeme wa kutosha kwa kila mmoja ili kutazama mechi.
Pamoja na kwamba, The Leopards , timu ya taifa ya Kongo – haikufudhu mashindano hayo, mashabiki wa mpira karibia nchi nzima hukaa kwenye makochi yao na kutazama kila mechi, na kufanya hali ya umeme nchini humo kuwa mbaya.
Kampuni ya umeme ya taifa, SNEL, imewaomba wateja wake siku ya leo Jumanne kuzima kila kitu watakavyoweza – yakiwemo majokofu, majiko na taa – ili taifa lisikatike umeme wakati wa mechi.
Wawakilishi wa kampuni hiyo hutokea kwenye televisheni kabla ya mechi na kuwaomba watazamaji kuzima vifaa visivyo vya lazima.
Ombi hilo limeonekana kuwakwaza wengi mjini Kinshasa.
“Hatuelewi kivipi… tunaombwa kuzima taa nyumbani, tusitumie majokofu au kitu chochote cha umeme,” alisema Michel Wandji.
Ila kuna wengine wamepokea ombi hilo. “Wakati wa mchana, huwa ni vizuri kuzima taa, ili uweze kuhifadhi umeme”, alisema Fabrice Mayama.
SNEL wameweka televisheni kubwa 16 katika miji ya nchi hiyo na kuahidi kuongeza nyingine 12 kwenye mji mkuu zikiwa katika jitihada za kuwaruhusu watu kutazama mechi katika njia ya kutunza umeme.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni