Sports and Entertainment

Jumatano, 25 Juni 2014

Duh eti hii ndio sababu ya Wema Sepetu kunyoa Para

Hakuna maoni :

Muigizaji wa Bongo Movie Wema Sepetu ameeleza sababu hasa iliyompelekea kunyoa nywele na kubaki na upara
Wema-anyoa-nywele
Wema ameuambia mtandao wa Bongo5 kuwa aliamua kunyoa nywele kwa lengo la kuigiza kama mgonjwa wa saratani kwenye filamu yake inaitwa FAMILY, aliyofanya na Aunt Ezekiel.
Amesema ameamua kuigiza filamu hiyo ili kuleta utofauti katika tasnia ya filamu Tanzania kwa kuwa anaona filamu nyingi za Tanzania zina masimulizi yanayofanana.
“Kwa sabababu unaweza ukashangaa mtu amekaa kwenye kochi yaani yeye story imeenda imerudi wako kwenye makochi tu sebuleni, wamehama sana wameenda chumbani, hawathink out of the box. Na story ni zilezile, mtu hawezi sijui kuzaa, kuna sijui uganga. Sisi tumefanya kwanza research, tukaangalia story ambayo iko different. Story ambayo hawajafanya watu wengi. Tumehit target nyingine, it’s about Cancer, kwenye hiyo story ni mgonjwa wa cancer na ndio maana kuna kipindi mliona nimenyoa kabisa kipara. Watu wengi walijiuliza kwa nini Wema kanyoa lakini the aim was kudeliver kile kitu ambacho nilitaka kudeliver kuwa kitu halisi.”

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni