Jumatano, 11 Juni 2014
David Luiz asaini mkataba wa miaka mitano PSG
mlinzi wa kibrazil David Luiz amejiunga na mabingwa wa Ufaransa Paris Saint-Germain.
Klabu yake ya sasa, Chelsea, na PSG wote wamethibitisha kwenye tovuti zao rasmi mwezi uliopita kukamilika kwa dili hilo lililogharimu pauni milioni 40.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka, ambaye anatarajia kuiongoza Selecao kutwaa ubingwa wa sita wa dunia katika ardhi ya nyumbani, amethibitisha atacheza katika Ligue 1 kwa misimu mitano ijayo.
"nimesaini mkataba na PSG kwa miaka mitano," alisema
"niliondoka Ulaya wakati nikiwa na miaka 18, nimepiga hatua chache ... tutaona. mipango ya leo inaweza kuwa isifae kesho. "
makamu nahodha huyo wa Selecao pia alizungumzia maandamano juu ya matumizi ya serikali kwa Kombe la Dunia.
"Kama kila kitu kiko sawa ni poa. Sitaki kuona ghasia, "alisema.
"sitaki Ulaya waseme vibaya kuhusu nchi yetu, Brazil ni mbaya. Brazil ina mambo mengi makubwa "
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni