Jumatano, 11 Juni 2014
Ronaldo arudi kuipa Uhai Ureno
Cristiano Ronaldo alicheza mechi ya kirafiki kabla ya kuanza mashindano ya kombe la Dunia huko Brazil katika ushindi 5 - 1 dhidi ya jamuhuri ya Ireland.Raul Meireles pia alirejea baada ya kuumia, akimpa matumaini kocha Paulo Bento uwanja mpana wa kuteua kikosi chake wakiwa katika kundi gumu lenye Ujerumani, Ghana na Marekani. Ronaldo alianza kwa uharaka mchezo huo dhidi ya jamuhuri ya ireland na kumfanya David Forde afanye kazi ya ziada.Portugal waliandika bao lao la kwanza kwa krosi ya Silvestre Varela kumkuta mfungaji Hugo Almeida alieparaza kwa kichwa na kumpita Forde. Ronaldo alikua akishangiliwa na umati wa watu wakati yeye alibisha hodi dakika ya 19 ambapo shuti lake liligonga mwamba. dakika tu baadaye Ureno walikuwa mbele 2-0 baada ya shuti la Fabio Coentrao kumgonga mlinzi Richard Keogh na kutinga wavuni. Ronaldo alitoa pasi ya goli la tatu katika dakika ya 37 wakati Almeida alipomfunga Forde baada ya kichwa cha nyota huyo wa Real Madrid kuokolewa. James McClean alifunga goli la kufutia machozi kwa vijana wa Martin O'Neill baada ya mapumziko, lakini Ureno waliongeza magoli kupitia Vieirinha na Coentrao.Luis Nani alifurahishwa kuona mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United amerudi,". Nadhani alionyesha yeye ni bora, yeye ni bora, na nadhani alionyesha atakuwa fit kwa asilimia 100" tupo katika kundi gumu lakini katika Kombe la Dunia unatakiwa ujue utakutana na timu bora.Tuko tayari na tuna ujasiri. "
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni