Sports and Entertainment

Jumamosi, 28 Juni 2014

Duh Nigeria wagomea mazoezi kushinikiza mafao

Hakuna maoni :

Kikosi cha Nigeria kinachoshiriki Kombe la Dunia kimeacha kufanya mazoezi kutokana na sakata linalohusu pesa ya ziada.
BBC Sport wanajua kuwa wachezaji hao wanaamini kuwa kila mmoja amekatwa dola 15,000 kwa kile walichoahidiwa kwa kufika hatua ya 16 nchini Brazil.
Wamekataa kufanya mazoezi huko Campinas siku ya Alhamisi na baadae maafisa wakakathibisha kuwa kipindi hiko kilisitishwa.
Nigeria wamepangwa na Ufaransa kwenye hatua ya mtoano ambapo watapambana siku ya Jumatatu.
BBC Sport pia wanajua kuwa tatizo limesababishwa na suala la pesa ya ziada, kwani wachezaji waliamini kuwa watapokea dola 10,000 kwa ushindi 1-0 dhidi ya Bosnia-Hercegovina na dola 5,000 kwa kutoa suluhu ya 0-0 na Iran.
Wachezaji hao wanaelewa kuwa walitakiwa kupewa dola 30,000 kila mmoja kwa kufudhu kutoka hatua ya makundi.
Sio mara ya kwanza kwa Tai hao kugoma kwa ajili ya pesa – mwaka uliopita walichelewa kuwasili katika mashindano ya Kombe la Shirikisho nchini Brazil.
Kweli pesa hazijai, mbele ya chapaa, utaifa hauna budi kusubiri kwanza…

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni