Ijumaa, 27 Juni 2014
Maximo ajifunga Jangwani Miaka Miwili
Aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya hapa nchini Maxio Maximo kutoka Brazil amepata fursa ya kurudi tena hapa nchini, kuja kuisuka vyema timu ya Yanga ili iweze kucheza katika michuano ya kimataifa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani, wakala aliyemleta Maximo, Ally Mlee alisema kuwa, ilimchukua miaka 3 kumuomba kuja hapa nchini kusuka timu ya yanga, kwa kujali kwake na ukarimu wa watanzania amekuja tena hapa nchini na amesaini mkataba wa miaka miwili.
Kwa upande wake Maximo alisema kuwa, amefurahi kuja kusuka timu ya yanga na anamatumaini itafanya vyema katika michuano mikubwa nje ya nchi lakini hata katika ligi ya hapa nyumbani.
“Watanzania ni wakarimu sana ndio maana nimekubali kuja tena hapa nchini kuinoa Yanga, lakini pia ujio wangu nimekuja na kocha msaidizi ambaye atanisaidia kusimamia na pia nitapendekeza wachezaji wazuri kutoka katika timu kubwa huko Ulaya, ili waje kuchezea Yanga lakini pia ni fursa kwa wachezaji wa yanga kujinoa kupitia wachezaji wakubwa,” alisema Maximo.
Siku ya Jumatatu timu ya Yanga itaanza mazoezi na mwalimu huyo mpya, maandalizi ya kujiandaa na ligi mbalimbali.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni