Sports and Entertainment

Ijumaa, 20 Juni 2014

Facebook yamtambua Diamond Platnumz

Hakuna maoni :

diamod
Gwiji wa muziki wa Tanzania ambaye sasa kila kona jina lake limekuwa midomoni mwa watu pengine kuliko msanii wa tasnia yoyote kwa sasa mara baada ya kutambulika na mtandao wa kijamii wa twitter ,facebook nayo imempa verification.
Hii ni neema nyingine kwa Diamond Platnumz, baada tu ya kuwa verifie kwenye mtandao wa twiter, hatimaye sasa kuwa Verified kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, hii inamaanisha kuwa kampuni ya Facebook hivi sasa inamtambua Diamond Platnumz kuwa kama msanii maarufu wa kimataifa, nafasi hii wanatokea kupata wasanii wachache sana na watu maarufu ambao wanapata bahati ya kujulikana na makampuni makubwa kama haya. Mwanamitindo wakimataifa Flaviana Matata ni mmoja wa watu maarufu watokao nchin Tanzania wanaotambuika na kampuni hiyo, na ni moja ya watu maarufu ambao account yao ipo Verified kama hii ya Diamond Platnumz. Huu ni mwaka mzuri sana kwa Diamond Platnumz kwa matukio yanayoendelea kumtokea, na kuzidi kumpa jina kubwa ulimwenguni kupitia muziki wake huu wa Style yake ya kipekee iliyopewa jina la AfroPop.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni