Ijumaa, 20 Juni 2014
Ndanda FC yadhaminiwa na Binslum
Timu ya mpira wa miguu ya Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya Binslum Tyre, pamoja na kupewa kitita cha milioni 50 ambacho kitawasaidia kununua vifaa mbalimbali vya michezo.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Nassoro Binslum alisema kuwa, wameamua kutiliana saini ya mkataba huo ili kuweza kukuza soka hapa nchini na kuwa na uwanja mpana wa kushindana ukiachana na timu zilizokuwepo kwa sasa za Azam Fc, Mbeya City, Simba na Yanga.
Binslum alifafanua kuwa anamatumaini timu ya Ndanda itakuwa kwa kiwango cha hali ya juu sana tofauti na zamani na kupelekea ushindani mkubwa sana.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Ndanda FC Edimund Kunyengana alisema kuwa, mkataba huo utawasaidia sana kuboresha mpira na kuwa na timu zingine ambazo kwa sasa ziko juu sana katika mpira hapa nchini.
“Nawatahadharisha timu zingine wajiandae kupambana na sie kwani baada ya kumaliza mkataba huo basi watakuwa wako juu kama timu zingine.” alisema Kunyengana
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni