Sports and Entertainment

Alhamisi, 26 Juni 2014

FIFA Kumfungia "Mwendazimu" Suarez miaka miwili

Hakuna maoni :
Suareza akimng'ata
Suareza akimng’ata Giorgio Chiellini
Uruguay imefanikiwa kusonga mbele baada ya kuinyuka Italia kwa goli moja kwa nunge kwenye mechi ambayo mshambuliaji hatari wa Uruguay na Liverpool, Luis Suarez alikutana na shutma nyingine ya kumng’ata mchezaji Giorgio Chiellini.
Straika huyo mtukutu anakabiliwa na adhabu kali ya kutoshuka dimbani kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kukosa mechio zilizosalia za michuano ya kombe la Dunia endapo atapatikana na hatia ya kumuuma meno mchezaji huyo wa Italia.
Shirikisho la kandanda FIFA limeanzisha harakati za kumuadhibu mchezaji huyo aliyemng’ata meno mchezaji mwenzie hapo jana ambapo Uruguay ikichomoza na ushindi wa bao 1 kwa bila hata hivyo Gelini amedai kuwa Suarez alimng’ata begani licha ya mruguay huyo kudai kuwa yeye ndiye aliyefanyiwa madhambi.
Chiellini akiugulia maumivu baada ya kuumwa meno na Straika huyo wa timu ya Taifa ya Uruguay na Liverpool
Chiellini akiugulia maumivu baada ya kuumwa meno na Straika huyo wa timu ya Taifa ya Uruguay na Liverpool
Suarez mwenye umri wa miaka 27 huenda akasimamishwa kutoshuka dimbani katika mechi 24 au kuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miaka miwili.
Mwamuzi aliyesimamia mecho hiyo kutoka Mexico, Marc Rodriguez hakuchukua hatua yoyote kufuatia kutoona kitendo hicho lakini FIFA bado inamamlaka ya kumuadhibu Suarez huku   klabu yake ya Liverpool imesema itakaa na kujadili mustakabali wa mchezaji huyo.
Hii sio mara ya kwanza kwa Suarez kufanya kosa kama  hilo, kwani hata mwaka jana aliwahi kumuuma meno mchezaji Branislav Ivanovic wakati Liverpool ilipoumana na Chelsea.
Suarez Uruguay
Straika Mtukutu, Luis Suarez akiugulia baada ya kumng’ata Chiellini
Wakati vioja hivyo vikiendelea, timu ya Taifa ya England imejikuta ikiaga mashindano hayo baada ya kubanwa mbavu na Costa Rica kwa suluhu isiyokuwa na goli.
Huku wawakilishi wa Afrika, timu ya Ivory Coast waliokuwa wanahitaji suluhu, kupoteza nafasi hiyo baada ya kufungwa goli dakika za majeruhi kwa mkwaju wa penalti na kujikuta wachezea kichapo cha mbili kwa moja na kuaga mashindano haya wakati Japan nao wakilambishwa mabao 4 – 1 dhidi ya vinara Colombia.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni