Alhamisi, 26 Juni 2014
Uruguay waja juu kuhusu Suarez
Chama cha mpira wa miguu cha Uruguay kimeingilia kosa ili kumuokoa Luis Suarez na adhabu ndefu kwa kumng’ata Giorgio Chiellini, kwa kudai kwamba Suarez ni mhanga wa kampeni chafu zinazofanywa na Waitalia, vyombo vya habari vya Uingereza na wenyeji Brazil.
Huku Suarez akipata presha kutoka kwa wadhamini, wachezaji wenzake pamoja na kamati ya nidhamu ya Fifa kwa kitendo cha kuzamisha meno yake kwenye bega la Chiellini, chama hicho kinajaribu kumaliza tatizo hilo salama.
Wakuu kutoka Adidas, kampuni ya vifaa vya michezo walisema kwamba wakati Suarez alipomng’ata mchezaji wa Chelsea Branislav Ivanovic na kufungiwa mechi 10, hiyo ilikuwa kumbukumbu kwa Suarez kuvuna alichopanda”, siku ya Jumatano walikutana mjini Rio kwa mazungumzo ya mgogoro huo. Kampuni ya Poker 888.com pia inaufanyia durusu mkataba wake na Suarez.
Kamati ya nidhamu ya Fifa, ambayo iko chini ya mwenyekiti ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Uswisi Claudio Sulser, alikuwa na kikao na chama cha soka cha Uruguay pamoja na Suarez siku ya Jumatano usiku, na amekipa muda wa kuwasilisha ushahidi wao.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni