Ijumaa, 20 Juni 2014
Mapenzi yachanganya makocha Brazil
Sayansi inaeleza kwamba mapenzi hakika yanasaidia, hayaumizi, uchezaji wa wanamichezo. Ila makocha wenye mashaka wamekataa.
Wakati unapoendelea kutazama tukio muhimu la michezo duniani, wala hupati nafasi ya kuujali mwili wako.
Wakati wataalamu wakikataa kuwa kufanya mapenzi kabla ya mechi kunaweza kuathiri uchezaji wa mchezaji, timu nyingi katika Kombe la Dunia wametekeleza kuzuia kufanya mapenzi.
“Hakutakuwa na kufanya mapenzi Brazil. Wanaweza kutafuta suluhisho jingine, wanaweza kupiga punyeto kama wanataka. Sipendi wanavyofanya makocha wengine, hii sio safari ya mapumziko, tuko hapa kucheza mpira kwenye Kombe la Dunia, alisema kocha wa Bosnia-Herzegovina, Safet Susic.
Siku ya Jumanne, Quartz lilitaja timu zenye sheria ya mapenzi Kombe la Dunia.
Timu zilizoruhusiwa kufanya mapenzi;
Ujerumani, Hispania, Marekani, Australia, Italia, Uholanzi, Uswisi, Uruguay na Uingereza.
Zilizokatazwa ni;
Urusi, Bosnia na Herzegovina, Chile na Mexico.
Sheria ni ngumu kwa timu hizi: Ufaransa (unaweza kufanya ila sio usiku kucha), Brazil (unaweza kufanya ila sio mapenzi ya akrobatiki), Costa Rica (hakuna mapenzi mpaka raundi ya pili) na Nigeria (unaweza kulala na mke ila sio mpenzi).
Sheria kwa timu nyingine hazijulikani.
Imani ya makocha na wachezaji
Wengi wao wanaamini kuwa kutofanya mapenzi kunamfanya mtu awe na hasira, imani inayotoka kwenye utamaduni wa zamani wa Wagiriki.
Muhammad Ali
Bingwa huyu wa masumbwi alikataa kufanya mapenzi wiki sita kabla ya pambano, akihofia kutoa shahawa kutamfanya aachie homoni (kisha hasira) ambazo zitahitajika kwa ajili ya mpambano wa ngumi.
Kiukweli, kinyume chake ndiko kulikothibitisha kuwa kweli. Tafiti zinaonyesha kuwa homoni hizo huongezeka baada ya kufanya mapenzi.
Maane yake ni kwamba mapenzi huongeza uchezaji zaidi kwa kuziachia hizo homoni mwilini.
Baadhi ya wataalamu wamehoji kuwa washindi wa Kombe la Dunia waliopita wanathibitisha kuwa ina manufaa.
“Timu ya taifa ya Uholanzi, kwenye Kombe la Dunia la 1978 nchini Argentina, ni kwamba mratibu wa wa michezo na mratibu mkuu Juan Carlos Medina wa idara ya Teknolojia ya Monterrey Mexico aliambia CNN.
“Baadhi ya wale wachezaji walisindikizwa na wake zao, na walishinda nafasi ya pili, sisemi kuwa ni kigezo muhimu, ila kinasaidia.”
Pele
“Hata yeye alikiri kuwa hakuweza kuacha kufanya mapenzi na mke wake kabla ya mechi, namaanisha, kwamba mapenzi yanasaidia kukutuliza, huo ndio ukweli,” aliongeza.
“Hatimaye ikiwa mapenzi yataleta athari mbaya kwa hisia za mtu kabla mchezo, hilo hutegemea na mtu binafsi. Wengine huona ni ahueni, wengine ni matatizo. Kijumla, mwanamichezo hapaswi kufanya chochote kabla ya mashindano muhimu ambacho hajawahi kukijaribu kwenye mashindano mepesi au mazoezi”, alihitimisha Shrier.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni