Ijumaa, 20 Juni 2014
Mourinho aitamani England
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amekubali kuwa anafikiria kuifundisha Uingereza hapo badae baada ya kuikataa nafasi hiyo hapo awali kutoka kwa Chama cha Soka Cha Uingereza (FA).
Mourinho alifuatwa kuchukua nafasi ya Steve McClaren baada ya kuondoka Chelsea Septemba 2007, ila alikataa nafasi baada ya kufuata ushauri wa mke wake Matilde, ambaye anaamini kuwa mumewe angeshindwa kushughulika kila siku kwenye uongozi wa klabu.
Mreno huyo alidai kuwa ipo siku moja atakuja kuwa kocha wa kimataifa.
Akiulizwa kama angependa kuifundisha Uingereza, Mourinho aliiambia ITV News ya London kuwa: “Ndio, ila sio sasa, sio miaka saba iliyopita nilipopewa na nafasi. Nilifanya maamuzi sahihi, mke wangu alinisaidia kufanya uamuzi sawia.
“Sio sasa. Hakuna jinsi, bado kijana, nguvu nyingi, hamu kubwa ya kufanya mazoezi kila siku, kucheza kila mechi, kucheza mara tatu kwa juma, bado hamu ipo”
“Ila naipenda nchi yako sana, tena sana. Niko nyumbani.”
“Bila shaka kitabu cha kusafiria hakibadiliki (pasipoti), moyo pia haubadiliki”
“Mimi ni Mreno asilimia 100, ila naipenda nchi yako, na kama siku moja nafasi itatokea, kwanini niikatae?”
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni