Alhamisi, 26 Juni 2014
Stephen Keshi : Jamani Messi ndugu zake wako Jupiter
Kocha wa Nigeria Stephen Keshi alisema Lionel Messi “anatoka sayari ya Jupiter” baada ya mshambuliaji huyo wa Argentina kufunga mara mbili na kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya taifa hilo la Afrika.
“Messi ni mchezaji noma. Amebarikiwa. Huwezi kuchukua kipaji chake”, alisema Keshi, ambaye kikosi chake cha Nigeria kiliweza kufudhu pamoja na kufungwa.
“Kuna wachezaji kama yeye kwenye timu ila Messi anatoka sayari ya Jupiter”.
Kwa sasa Messi ndiye anayeoongoza kwa ufungaji kwenye mashindano ya 2014 akiwa na magoli manne, pamoja na Neymar wa Brazil. Kabla ya Brazil, 2014, aliwahi kufunga goli moja tu katika mechi nane za Kombe la Dunia.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni