Sports and Entertainment

Jumanne, 15 Julai 2014

cararragher : mnunueni Ronaldo aje azibe pengo la Suarez

Hakuna maoni :


Mlinzi wa zamani wa Liverpool  Jamie Carragher 36, amedai kuwa hana imani kama ‘The Reds’ itatoa upinzani mkubwa katika kugombania taji la Ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao wa 2014/2015.
Carragher ameyasema hayo mara baada ya Livepool kuiachia mashine yao ya  kufyatua magoli Luis Suarez 27, kuhamia klabu ya Barcelona kwa ada ya pauni milioni 75 ambazo ni sawa na mkwanja mrefu  wa shilingi bilioni 187.5 za kibongo.
Hata hivyo klabu hiyo kutoka Anfield imeonekana kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa 2014/2015 kwa kufanya usajili pamoja na kuingia katika mazungumzo na baadhi ya klabu kwa madhumuni ya kupata huduma za mastaa mbalimbali.
“Sidhani kama Liverpool watang’aa katika msimu ujao, pengo la Suarez siyo rahisi kuzibika labda ufanyike usajili wa Cristiano Ronaldo au Lionel Messi katika klabu hiyo”, alisema nahodha huyo wa zamani wa Liverpool.
Ila aliendelea kutiririka  kuwa;  lolote linaweza kutokea msimu ujao, kwani hakuna mtu aliyeweka ‘mzigo’ kubashiri kama kikosi cha Brendan Rodgers wangeshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita wa 2013/2014.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni