Sports and Entertainment

Jumanne, 15 Julai 2014

TETESI ZA USAJILI MAJUU

Hakuna maoni :

Kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, amewapa matumaini zaidi Manchester United baada ya kukiri kuwa "angependa kuichezea moja ya klabu kubwa duniani"

ingawa amesema hatolazimisha uhamisho wake (Independent) United pia wamepata matumaini baada ya winga wa Real Madrid, Angel Di Maria, 26, kukataa kwenda Paris St- Germain (Daily Mirror), beki wa Atlètico Madrid, Filipe Luis, 28, anajiandaa kufanya vipimo vya afya kabla ya kuhamia Chelsea kwa ada ya pauni milioni 20 (Daily Express), boss wa Sevilla Unai Emery amesema anajiandaa kumpoteza beki wake wa kushoto Alberto Moreno, 22, ambaye anasakwa na Liverpool (Talksport), mshambuliaji wa Paris St-Germain Edison Cavani, 27, amemtaka wakala wake kumtafutia timu katika Ligi Kuu ya England (Sky Sports), Arsenal wapo tayari kuacha kumfuatilia kiungo wa Real Madrid Sami Khedira, 27, kufuatia kudai mshahara mkubwa. Khedira anataka kuwa mchezaji anayelipwa zaidi Emirates (Daily Mirror), Arsenal wanaongeza ufuatiliaji wa beki wa kulia wa Southampton Calum Chambers, 19, licha ya kuwa wanakaribia kumchukua Mathieu Bebuchy, 28, kutoka Newcastle (Daily Mail), beki wa zamani wa Manchester. United Rio Ferdinand, 35, atasaini kuichezea QPR siku ya Jumanne (Sky Sports), Liverpool huenda wakipanda dau la pauni milioni 44 kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Marco Reus, 25, (Daily Express), Dynamo Moscow wamekubaliana na Marseille kumsajili Mathieu Valbuena, 29, kwa pauni milioni 5.5. Arsenal, Tottenham na West Ham zilikuwa zikimtaka pia (Talksport), Robin Van Persie amepewa wiki tatu za kupumzika na Manchester United baada ya Kombe la Dunia, huku Wayne Rooney wa Engalnd akitakiwa kuripoti kambini mapema (Sun), kiungo wa Arsenal Jack Wilshire, 22, aliyeomba radhi mwezi Oktoba kwa kuonekana akivuta sigara, ameonekana tena akifanya hivyo mjini Las Vegas akiwa na Joe Hart (Daily Mail), Arsenal watataka Chris Smalling kujumuishwa kwenye mkataba wowote iwapo Manchester United watamchukua Thomas Vermaelen (Metro) Newcastle wamekamilisha usajili wa Daryl Janmaat wa pauni milioni 5, kuziba nafasi ya Mathieu Debuchy (Guardian). Share tetesi na wapenda soka.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni