Alhamisi, 24 Julai 2014
duh eti TRA TABORA Imevuka maengo ya ukusanyaji mapato
Mamlaka ya mapato nchini (TRA) mkoani Tabora imefanikiwa kuvuka lengo iliyopewa na serikali la kukusanya shilingi bilioni 15.1 na kufikia bilioni 15.4 sawa na asilimia 102%, katika mwaka wa fedha uliopita wa 2013, hiyo ikibainishwa kuwa imetokana na mausiano mema baina ya mamlaka hiyo na walipa kodi.
Hayo yamebainishwa na meneja wa mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Tabora Bw. Laurent Paulo katika hafra fupi ya futari iliyoandaliwa na mkurugenzi mkuu wa fedha TRA Bw. Salehe Mshoro, wakati akifuturisha wadau wa TRA mkoani Tabora, ukiwa moja ya mikoa minne ambayo TRA imefururisha kwa mara ya kwanza mwaka huu ambayo ni Arusha, Tanga, Kagera na Tabora.
Akizungumza na wadau wa TRA walioshirikia katika futuru hiyo mjini Tabora, mkurugenzi wa fedha TRA Bw. Salehe Mshoro amesema kuwa, mamlaka imepewa jukumu la kukusanya zaidi ya trilioni 11, ili ifikie lengo unahitajika mshikamano wa TRA na wadau kama walivyofauru mkoani Tabora iwe ni mfano kwa taifa zima.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tabora aliyekuwa mgeni rasmi katika futuru hiyo, katibu wa afya mkoa wa Tabora Bw. Hamis Dinya amesema kuwa, fursa hiyo iliyotolewa na TRA iwe mfano wa kuigwa kwa mashirika yanayotoa huduma katika jamii, na kuelekeza misaada hiyo kwa jamii, ambayo ni wazee wasiojiweza, na watoto yatima.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni