Sports and Entertainment

Alhamisi, 24 Julai 2014

Brazil yala matapishi yake kwa dunga

Hakuna maoni :

Brazil imemteua mchezaji wa zamani Dunga kuwa kocha mpya kwa mara ya pili.
Dunga alikuwa nahodha wa Brazil kwenye ushindi wa Kombe la Dunia 1994 na aliwahi kuwa kocha wa timu hiyo kuanzia 2006 mpaka 2011.
“Nina furaha kubwa ya kurudi”, alisema kocha huyo,50, ambaye alipendekezwa kufanya kazi hiyo.
Dunga anachukua nafasi ya Luiz Filipe Scolari, ambaye alijiuzulu baada ya Brazil kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia na kuchezea kichapo kikali cha kihistoria kwa kufungwa 7-1 na Ujerumani.
Dunga alikuwa na timu hiyo kwenye Kombe la Dunia la 2010 nchini Afrika Kusini ambapo Brazil ilitolewa kwenye robo fainali.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni