Jumatano, 30 Julai 2014
Jeshi la Polisi Kagera lakamata shehena ya vipodozi haramu.
Jumla ya maboks miatano sitini na nane yamekamatwa na jeshi la polisi Kagera yakiwa na vipodozi haramu pamoja na dawa za binadamu.
Akiongea mkoani Kagera kamanda wa jeshi la polisi wa mkoa huo Henri Mwaibambya amesema vipodozi hivyo vilikamatwa katika tarafa ya bugabo wilayani Bukoba vikiwa ndani ya ziwa victoria vikiwa vimeingizwa nchini kutoka nchi jirani ya Uganda kwa njia ya magendo huku vikiwa vimepakiwa ndani ya mtumbwi wa mbao wenye namba za usajili TMZ 010078, ambapo amewataja watuhumiwa walio kamatwa kuwa ni Otanga Jaluo-miaka 34 mkazi wa Pasiasi Mwanza, Yusuph Juma-miaka 46 mkazi wa Mwanza na Eleven Sylivester Msimbiti -miaka 43 mkazi wa Mwanza.
Aidha kamanda huyo wa jeshi la polisi amethibisha kutokea kwa kifo cha mauaji ya mtoto mchanga mwenye umri wa miezi tisa aitwae Angel Abeid, ambae ameuawa usiku wa kuamkia leo na mama yake mzazi Vaileth Kalumuna-miaka18, ambapo ameongeza kuwa mama huyo alimbana pua na mdomo wa mtoto huyo hadi akapoteza maisha, na baada ya kuhojiwa na jeshi la polisi mama huyo alieleza chanzo cha kumuua manae kuwa ni ugumu wa maisha.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni