Sports and Entertainment

Ijumaa, 4 Julai 2014

Jeshi la polisi mkoani Mara lawashikilia askari wake watatu kwa tuhuma ya mauaji.

Hakuna maoni :

Jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya,linawashilia askari wake watatu kwa tuhuma za kumpiga  hadi  kumuua  kijana mmoja  Kitandika Ryoba  mkazi  wa Sirari,baada  ya  kumkamata  kwa  madai  ya  kumkuta  akivuta  bangi  na  kucheza  kamali  katika  eneo  hilo la  Sirari  mpakani  mwa Tanzania na  Kenya.
Jeshi hilo la polisi limechukua hatua hizo siku chache tu baada ya mamia ya wananchi wa mji huo mdogo wa Sirari kufanya vurugu na maandamano makubwa  huku wakichoma tairi za magari katika barabara kuu ya Sirari,Tarime -Mwanza,vurugu ambazo zililenga  kulitaka jeshi hilo kueleza chanzo cha kifo cha kijana huyo,anayedaiwa  kuuawa kisha mwili wake kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha  maiti cha hospitali ya wilaya ya Tarime bila ya ndugu na jamaa zake  kujulishwa kuhusu tukio hilo.
 
kamanda wa polisi wa kanda maalum  ya Tarime na Rorya kamishina  msaidizi mwandamizi  wa  polisi Justus Kamugisha,amesema jeshi  hilo linawashikilia askari wake hao watatu kwa mahojiano ambao   walimkamata kijana huyo kabla ya kuuawa kwa kipigo, wakati jeshi hilo  likisubili majibu ya uchungizi wa sehemu ya mwili wa marehemu  ambayo yamepekelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali.
 
Wakizungumza katika  mazishi  ya  kijana huyo, ambayo yamefanyika  katika mji mdogo wa Sirari,baadhi  ya viongozi  wa halmashauri ya wilaya ya Tarime na vyama vya siasa,wamewataka askari wa jeshi hilo kubadilika katika utendaji wao wa kazi, kwani wamesema kitendo  cha  polisi  kuua ovyo raia kwa kisingizi kuwa ni watuhumiwa kinachochea chuki kati ya jamii na jeshi hilo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni