Sports and Entertainment

Ijumaa, 4 Julai 2014

Tani 20 za takataka huingia baharini kila mwaka

Hakuna maoni :


Utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira – UNEP umeonyesha kuwa TANI milioni 20 za taka za plastiki huingia baharini kila mwaka duniani kote.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini NAIROBI, KENYA mtafiti mkuu wa UNEP, JACQUELINE McGLADE amesema taka hizo husababisha uharibifu mkubwa baharini yakiwepo maeneo ya mazalia ya samaki.

Amesema taka za plastiki zinazoingia baharini husababisha hasara ya zaidi ya dola MAREKANI milioni 13 kila mwaka duniani kote.

Baadhi ya taka za plastiki zinazoingia baharini ni pamoja na nyavu za uvuvi chakavu ambazo huachwa na wavuvi baharini, mifuko ya plastiki ambayo hupelekwa baharini na maji ya mvua na upepo mkali na kuhatarisha maisha ya samaki baharini.

Madhara mengine ni magonjwa ya njia ya hewa yaletwayo na moshi wa taka hizo za plastiki zinapochomwa moto ovyo katika maeneo ya makazi.

Katika mkutano huo Mkurugenzi mtendaji wa UNEP, ACHIM STEINER ametoa wito kwa serikali duniani kusimamia ipasavyo utekelezaji wa sheria za mazingira na sera zinazohusu matumizi na utengenezaji wa vifaa na mifuko ya plastiki ili kupunguza matatizo yaletwayo na matumizi ya vifaa vya plastiki.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni