Jumatatu, 7 Julai 2014
JWTZ Yafunika sabasaba
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetia fora kwa kutoa huduma ya afya kwa wakazi wapatoa 10,000 kwa magonjwa mbalimbali.
Akizungumza na Taarifa News Afisa Habari wa Jeshi hilo Luteni Kanali Erick Komba alisema kuwa, wakazi wengi wamepatiwa huduma mbalimbali katika banda hilo kwa sababu hakuna hospitali ya kutoa huduma ya afya.
Luteni Kanali Komba alitaja huduma zilikuwa zinatolewa katika banda hilo kuwa ni huduma ya macho, upigwaji miyale, maralia, HIV, mshtuko wa moyo, kisukari na utoaji dawa.
Kivutio kikubwa katika banda hilo ni kuhusu komando aliyebeba vifaa vya kikomandoo zaidi ya kilo 50 kama anakwenda kwenye vita, wiki ijayo kutakuwa na kongamano la kisheji ambalo JWTZ watajadili mambo mbalimbali ya kukabiliana na uharamia lakini pia Septemba 1 JWTZ watatimiza miaka 50 ya kuanzishwa kwake.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni