Sports and Entertainment

Jumanne, 8 Julai 2014

REST IN PEACE DI STEFANO

Hakuna maoni :

Gwiji wa soka Alfredo Di Stefano aliyeziwakilisha timu za Argentina,Colombia,na Hispania katika michuano ya kimataifa amefariki Dunia baada ya kupata shambulio la moyo.
Nyota huyo anayetambulika kama Nembo ya klabu ya Real Madrid amefariki akiwa na umri wa miaka 88.
Raisi huyo wa heshima wa klabu ya Real Madrid alipata shambulio hilo la moyo siku ya Jumamosi karibu na mitaa iyopo Santiago Bernabeu,siku moja baada ya sherehe yake ya kuzaliwa na kutimiza umri wa miaka 88,mauti yalimfika siku ya leo Jumatatu baada ya hali yake ya kiafya kuzorota gafla..
Di Stefano alianza kipaji chake cha soka akicheza klabu ya River Plate na baadae akahamia Madrid ambapo awali akitokea klabu ya Millonarios ya nchini Colombia mwaka 1953,katika kipindi hicho alikaribia pia kujiunga na Barcelona.
Gwiji huyo aliiwezesha klabu yake ya Bernabeu kubeba mataji nane ya Liga na makombe matano ya European Cups kati ya miaka 1953 na 1964
Mkalii huyo wa magoli aliweza kufunga magoli 308 katika mechi 396 alizocheza nakushika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora wa klabu hiyo nyuma ya Raul Gonzalez Blanco mwenye  rekodi ya magoli 323.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni