Jumanne, 15 Julai 2014
Man U kama uholanzi vilee : Van Gaal
Kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal ana matumaini ya kuunda umoja mkubwa ndani ya kikosi baada ya kuagiza wachezaji kula pamoja kila siku baada ya mazoezi.
Ni jambo la lazima kwa nyota wa United kukaa meza moja na wachezaji wadogo pamoja na timu ya makocha Carrington saa 7 mchana. Agizo hilo limekuja wiki hii baada ya kutarajiwa kuwasili kwa Van Gaal kwenye kiwanja cha mazoezi siku ya Jumatano asubuhi.
Raia huyo wa Uholanzi, 62, alizungumza mwishoni mwa wiki hii kuhusu mipango yake ya kuendeleza umoja na mshikamano kwenye kikosi cha United ambao uliisaidia Uholanzi kushinda nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia.
“Ni matumaini yangu kuwa United itakuwa kama Uholanzi”, alisema.
Kulikuwa na taarifa za kuwep[o na kuendeleza makundi msimu uliopita kwa kisa cha Sir Alex Ferguson kutaka kustaafu, ila Van Gaal amepanga kuwa wachezaji wake wote wawe kitu kimoja.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni