Sports and Entertainment

Jumanne, 15 Julai 2014

PAPA BENEDICTO XVI ACHEKELEA UBINGWA WA DUNIA KWENDA KWA WAJERUMANI

Hakuna maoni :

Papa mstaafu wa kanisa katoliki,  Benedict wa 16, (87), amesema amefurahishwa na ushindi walioupata Ujerumani kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil  kwasababu katika kikosi hicho wapo wachezaji wenye asili ya jimbo la Bavaria ambako ni sehemu alikozaliwa na kukulia.
Pia alituma salamu zake za kuwapa pole na kuwafariji mashabiki wa Argentina wakiongozwa na Papa Francis na kuwaombea ili wasahau mapema kipigo hicho walichokipata kutoka kwa watoto wa chancellor Angela Merkel.
Hata hivyo, wasemaji wa mkuu huyo wa zamani wa kanisa katoliki wameeleza kuwa Papa Benedict 16 ambaye ni mpenzi wa muziki wa piano aliamua kwenda kulala badala ya kuangalia fainali hiyo katika televisheni ingawaje wafanyakazi wote katika ofisi yake walikuwa wakimuunga mkono katika kushabikia timu ya taifa ya Ujerumani.
Hazikuwepo taarifa zozote kutoka katika ofisi ya Papa Francis, kufuatia kushindwa kwa Argentina katika hatua ya fainali ikumbukwe kiongozi huyo wa kanisa Katoliki Duniani ni mshabiki mkubwa wa kikosi cha Alejandro Sabella.
Mbali na utani mwingi kuhusiana na maswala ya soka baina ya Mapapa hao wa kanisa katoliki,  pia imeonekana watu hao wawili wana mahusiano mazuri, tofauti na baadhi ya watu wanavyowakuchulia
Asiyekubali kushindwa siyo mpinzani,  ‘ Ex-papa goli 1 na Papa goli 0’.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni