Ijumaa, 25 Julai 2014
Mario Mandzukic ajiunga na Atletico Madrid
Mara baada ya klabu ya Atletico Madrid kumtangaza Mario Mandzukic 28, kama mrithi mpya wa nafasi ya Diego Costa 25 aliejiunga na kikosi cha Chelsea, straiker huyo ameibuka na kuwaonya mashabiki klabu hiyo juu ya kulinganishwa kiuwezo na Costa
‘Costa ni Costa na Mario ni Mario kila mtu anayostaili yake ya uchezaji, najua anauwezo mkubwa lakini mimi pia ni mchezaji mkaali
Sipendi mashabiki wanifananishe naye, binafsi ninge penda kufananishwa na kocha wangu wasasa(Diego Simeone) nahisi yeye ndoi mshindani wakweli
Msimu uliopita alikuwa nafanikio mazuri yaliyosababisha Dunia imwamini, kwanza alifanikiwa kuvunja utawala wa Barcelona na Real Madrid kwa kuchukua taji la La Liga afu pili akafanikiwa kufika hatua ya fainali za Uefa champions league japokua hakufanikiwa kubeba kombe hilo
Lakini ikumbukwe kwamba hakua na wachezaji wa bei ya juu wakati alipokuwa akipata mafanikio hayo. Kwangu mimi huyo ndio shuja wa kweli ambaye ningependa kufananishwa nae
Diego Simeone alikuwa mchezaji bora katika enzi zake na ubora aliokuwa nao kipindi anacheza soka ndio huhuo alionao katika ufundishaji wa soka ndio maana nilifurahi kusikia alikuwa akinihitaji katika kikosi chake msimu ujao wa 2014/2015
Naamini nikiwa chini yake uwezo wa kutetea taji letu la ligi kuu tunao na pia kuufuta utawala wa muda mrefu wa vilabu viwili(Real na Barca) ‘.
Aliyazungumza hayo wakati wa mahojiano na mtaandao wa klabu, mara baada ya sherehe za kumtambulisha staa huyo kufanyika katika uwanja wa klabu wa Vicente Calderon jijini Madrid
Ambapo staa huyo alisajiliwa kwa ada ya euro milioni 15(Tshs bilioni 33) akitokea klabu ya Buyern Munich mara baada ya kudaiwa kukosana na kocha Pep Guardiola ikiharifiwa kuwa alikuwa akipinga majukumu aliyokuwa akipewa pamoja na falsafa za Mhispania huyo
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni