Sports and Entertainment

Jumapili, 6 Julai 2014

Mourinho : Silva ni muhimu bwana ,,, Neymar kitu gani?

Hakuna maoni :

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amedai kuwa, mlinzi Thiago Silva ndio mtu muhimu  katika kikosi cha Brazil zaidi ya Neymar, kocha huyo anaamini kwamba Brazil wamtamkosa mtu muhimu katika hatua hiyo ya nusu fainali watakapokutana na Ujerumani, akasisitiza kuwa Dante anapaswa kuonyesha kiwango cha juu ili kuziba pengo la Thiago Silva.
Nahodha huyo wa Selecao alifunga bao la kwanza katika mechi ya robo fainali dhidi ya Colombia kabla ya kupewa kadi ya pili ya njano, jambo linalomfanya ashindwe kucheza mechi inayofata dhidi ya Ujerumani.
Nyota wa Selecao Neymar atakosa mechi zote zilizobaki baada ya kupata maumivu makali ya mgongo katika mechi iliyopigwa siku ya Ijumaa, lakini Mourinho anaamini kuwa Brazil wanapaswa kuhuzunika baada ya kumkosa Thiago Silva zaidi ya Neymar kwa sababu pengo la mlinzi huyo ni vigumu kuliziba.
Aliendelea kutoa maoni yake katika gazeti maarufu la michezo la Hispania Marca, kwa kusisitiza kuwa Brazil wanamhitaji Neymar kwa sababu ni hodari akiwa uso kwa uso na mlinda mlango, pia anaweza akacheza vizuri mipira ya adhabu na kuweza kufunga kwa umahiri mzuri.
Hatahivyo amedaikuwa anaamini kuwa mchezaji wa Napoli, Henrique anaweza akaziba pengo lililoachwa na Neymar, huku Dante akicheza nafasi iliyoachwa wazi na Thiago ambapo atachuana na wachezaji wengi aliozoea kucheza nao akiwa katika timu ya Bayern Munich, pamoja na wachezaji wengine wa Bundesliga.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni