Jumapili, 6 Julai 2014
Uholanzi yatinga nusu fainali
Kocha wa timu ya Taifa ya Uholanzi, Luis Van Gaal amekiwezesha kikosi chake kutinga katika hatua ya nusu fainali mara baada ya goli kipa wa timu hiyo, Tim Krul kuibuka shujaa wa mchezo kwa kuweza kuzuia mkwaju miwili ya penalti toka kwa Bryan Ruiz na Michael Umana wa Costa Rica.
Mchezo mwingine wa hatua ya robo fainali uliochezwa hapo jana ni ulioikutanisha miamba miwili, Argentina iliyoitupa nje Ubelgiji kwa kipigo cha bao moja kwa nunge katika mtanange uliopigwa kwenye dimba la Estadio Nacional De Brasilia, huku goli pekee na la ushindi kwa Argentina likiwekwa kimyani na mshambuliaji wa klabu ya Napoli ‘Gonzalo Higuain’ na kuweka rekodi nyingine ya kutinga hatua ya nusu fainali tangu ifanye ivyo miaka 24 iliyopita.
Kwa matokeo hayo, Argentina pamoja na Uholanzi zimeweza kufuzu katika hatua ya nusu fainali ambapo zinatarajia kuvaana Julai 09 kwenye dimba la Arena De Sao Paulo wakati wenyeji Brazil watapimana nguvu na Ujerumani katika hatua hiyo jumanne ijayo.
Inaelezwa kuwa hizi ni fainali za 20 kufanyika zikiwa tayari zimekwisha shirikisha zaidi ya mataifa 23, ukiacha mataifa ya mwaka huu ambayo yamekwishachuana katika hatua ya mikwaju ya penalti na mara ya kwanza mikwaju ya penalti kutumika kwenye kombe la Dunia ilikuwa ni mwaka 1982 katika fainali zilizofanyika nchini Hispania huku takwimu zikionyesha zaidi ya mikwaju 140 imepigwa na zaidi ya asilimia 75 ya mikwaju hiyo imepelekea ushindi kwa timu ambazo zimeshinda mojawapo ikiwa ni Uholanzi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni