Alhamisi, 24 Julai 2014
TANZANIA NDIO NCHI YENYE RUTUBA ZAIDI UKANDA HUU
Imeelezwa kuwa asilimia 46 ya Ardhi yenye rutuba katika Jumuiya ya Afrika Mashariki inapatikana hapa nchini Tanzania, na ndio nchi inayotegemea kwa kilimo na kulisha nchi jirani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Mwenyekiti wa Tanzania Agriculture Society, Engerbert Moyo alisema kuwa, Tanzania ina ardhi kubwa sana ambayo bado haijatumika hata mara moja, lakini pia nusu ya ardhi yenye rutuba iko Afrika.
Moyo alifafanua kuwa asilimia 70 ya watu Bilioni 7 duniani kote wanategemea kupata chakula kutoka kwenye kilimo kwa nchi za Afrika.
Kwa upande wa Tanzania ni asilimia 30 ya watu wake wanategemea kilimo, siku ya Agosti 1 ni siku ya Kitaifa ya wakulima na wafugaji nanenane, kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Matokeo Makubwa Sasa Kilimo ni Biashara.’
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni