Sports and Entertainment

Alhamisi, 24 Julai 2014

Boko haram wadaiwa kulipua daraja

Hakuna maoni :


Wanamgambo wa Kiislamu wanashukiwa kulipua daraja kuu lililopo kaskazini mashariki, wakikwamisha mawasiliano ya usafiri na Cameroon, walisema wakazi wa hapo.
Magari na malori yenye mizigo yamekwama barabarani na kushindwa kupita daraja la Ngala, wakazi hao waliiambia BBC.
Shambulio hilo lililofanyika usiku linaonyesha kukua kwa hofu kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Boko Haram, alisema mwandishi wa BBC.
Siku ya Jumanne, mkuu wa majeshi alisema baadhi ya wanajeshi walitoweka kwa sababu walikuwa wanawaogopa Boko Haram.
Wanajeshi hao walijiunga na jeshi kimakosa, alisema Luteni Jenerali Minimah.
Mwandishi wa BBC Bashir Sa’ad aliyeko jijini Abija, anasema maoni yake (Jenerali Minimah)yanatoa picha ni kwa namna gani jeshi limeshndwa, limekosa hamasa au nguvu ya kupambana na Boko Haram.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni