Jumanne, 22 Julai 2014
Wabrazil wampania mbaya wa Neymar
Mlinzi wa timu ya taifa ya Colombia Camilo Zuniga ametoa madai mapya juu ya kupokea vitisho na lugha chafu kutoka kwa mashabiki wa soka wa Brazil kwa kupitia simu yake ya mkononi pamoja na barua pepe (email), kufuatia rafu mbaya aliyomchezea Neymar 22, katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia lililofanyika Brazil
Katika mechi hiyo timu ya Brazil iliondoka na ushindi wa magoli 2-1 na kutinga nusu fainali , lakini mshambuliaji waotegemezi Neymar hakuweza kuendelea na michuano hiyo mara baada ya kuvunjika uti wa mgongo pia mlinzi wao tegemezi Thiago Silva alipata adhabu ya kukosa mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya kupokea kadi mbili za njano
Camilo Zuniga anayecheza katika klabu ya soka ya Napoli ya nchini Italia amedai kuwa sasahivi hajisiki kuwa huru anapotembea mitaani kama zamani jambo lililomfanya aanzekutembea na ‘Bodyguard’ kwa ajili ya usalama wa maisha yake
Hapo awali Neymar alikiri kuombwa msamaha na mlinzi huyo kwa kupitia mazungumzo ya simu ya mkononi, na akawa amekubali kumsamehe, lakini mashabiki wengi wa Brazil wanaamini kama siyo mlinzi huyo kumuumiza Staa wao ambaye alikosa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani, wasingeweza kupokea kipigo cha aibu cha magoli 7-1
Kwasababu kutokuepo kwa Neymar katika mchezo huo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia lilikuwa ni pigo kubwa kwa taifa lao na pia hata mzuka wa kikosi kizima ulishuka kwakuwa timu yao imeundwa katika mfumo wa kumtegemea staa huyo anayecheza katika klabu ya Barcelona
Inaonekana mashabiki wa Brazil wameamu kuhamishia hasira zao kwa beki huyo wa Colombia, lakini katika maoni ya wachambuzi wengi wa soka wanadai hatakama Neymar angekuepo katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani bado asingewasaidia lolote kwasababu kikosi chao hakikua na ubora wowote ukilinganisha na timu za Uholanzi, Argentina na mabingwa wapya wa Dunia katika soka, timu ya Ujerumani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni