Jumamosi, 2 Agosti 2014
Ancelotti : Man U Kurudi kileleni mapema? Hapana
Kocha wa zamani wa Chelsea Carlo Ancelotti ametabiri kuwa na changamoto kwenye msimu wa kwanza wa Ligi Kuu kwa kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal, kwa mujibu wa Daily Mirror.
Mtaalamu huyo wa Kiitalia, ambaye kwa sasa ni kocha wa Real Madrid, anaamini kuwa mashujaa hao wa Ligi ya Uingereza wanatakiwa kuwa washindani kuliko kawaida, na japokuwa van Gaal ni kocha mzuri na mwenye uzoefu, atajikuta kwenye kazi yenye mtego ya kuijenga klabu hiyo baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson.
“Ni kocha mzuri na mwenye uzoefu, ana uzoefu wa pekee na atafanya kazi nzuri United,” alisema. Ni kocha ambaye anajua kila kitu.”
“Sir Alex Ferguson, ilikuwa ngumu kwa United, ila kwa sasa wanapaswa kuijenga timu.”
“Wamesajili wachezaji wazuri, ila kuijenga timu sio jambo rahisi na Ligi Kuu ni ligi yenye ushindani sana.”
“Haitokuwa rahisi kushinda kwa mwaka wa kwanza, kwa sababu kuna timu nyingi zenye ushindani zinazotaka kushinda.”
Iliripotiwa kuwa Ancelotti alikuwa mmoja wa waliotafuta kazi ya ukocha msimu huu kabla timu hiyo haijaamua kumchukua van Gaal, na makocha hao watapambana leo kwenye mechi ya kirafiki.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni