Ijumaa, 1 Agosti 2014
AY,YAYA TOURE KUKUTANA NA OBAMA KUIMARISHA UHUSIANO WA MAREKANI NA AFRICA
A.Y akiwa na wasanii wengi wakubwa kutoka Africa watasafiri pamoja na mchezaji wa Manchester city “Yaya Toure” kwenda Washington D.C kwa ajili ya mkutano utakaofanyika kati ya tarehe 4 hadi 7 mwezi wa 8.
Safari hii ni kwa ajili ya shughuli za One Campaign ili kushiriki kutoa mchango wa kuimarisha mazungumzo kati ya serikali ya Marekani na nchi za Africa kwenye US-Africa Leaders Summit.
Rais Barack Obama atawakaribisha viongozi kutoka Africa kwenye mkutano wa siku tatu ambapo kwenye safari hii, wasanii watakuwa pia na mkutano na viongozi wa juu wa Marekani,wengine ni kutoka Young African Leaders Initiative (YALI) na members of congress.
Kwenye mikutano hii wasanii kwa pamoja watafanya utetezi na kusisitiza wananchi wa Africa kuchukua hatua za kujihusisha na kilimo kama ONE campaign inavyosisitiza. Zaidi ya kushiriki kwenye mkutano wasanii watafanya show kwa kuimba wimbo wa Cocoa Na Chocolate.
Listi ya wasanii ni A.Y. (Tanzania), Buffalo Souljah (Zimbabwe), D’Banj (Nigeria), Fally Ipupa (DRC), Femi Kuti (Nigeria), Judith Sephuma (South Africa), Omawumi (Nigeria), Victoria Kimani (Kenya) na Wax Dey (Cameroon).
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni