Ijumaa, 1 Agosti 2014
liverpool waongeza nguvu kwenye usajili, mbioni kukamilisha wengine wawili
Klabu ya Liverpool ipo mbioni kukamilisha uhamisho wa mastaa wawili kwa mpigo kutoka katika vilabu vya Atletico Madrid na Sevilla vya nchini Hispania.
Tayari mkurugenzi wa klabu hiyo Ian Ayre yupo nchini Hispania kujaribu kufanya mazungumzo na klabu ya Sevilla juu ya usajili wa beki Alberto Moreno 22, mwenye thamani ya pauni milioni 20 (Tshs bilioni 50).
Pamoja na kufanya makubaliano na klabu ya Atletico Madrid kumchukua Javi Manquillo kwa mkopo wa miaka miwili ambapo klabu hiyo inatarajia kumsajili moja kwa moja baada ya muda wa mkopo huo kuisha.
Akizungumza na mtandao wa klabu Bosi huyo amedai kuwa niya yao ni kutumia zaidi ya pauni milioni 100 (Zaidi ya Tshs bilioni 250) kwaajili ya usajili msimu huu wa majira ya joto.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni