Jumapili, 3 Agosti 2014
Havard yavurunda tena ubora wake washuka
Chuo cha Williams ndio chuo bora Amerika kwa sasa, hiyo ni kwa mujibu wa Takwimu za Vyuo bora kwa mwaka vya Forbes, ambapo kwa mwaka huu Chuo Kikuu cha Harvard kimeshika nambari saba.
Forbes, ambayo huonganisha vyuo vya sanaa na vyuo vikuu vya utafiti kwenye orodha yake, imegundua kuwa mgawanyo kati ya aina mbili za taasisi inadhihirisha kukua kwa elimu ya juu.
Pia, mjadala kuhusu matumizi ya shahada ya chuo yamepungua kuhusiana na sifa ya taasisi husika, zaidi ni kuzingatia masomo ya mwanafunzi. Orodha ya Forbes inaonyesha kwamba ni jambo zuri kama sio aula kusoma shule vyuo vidogo.
Kwenye orodha ya Forbes, chuo cha Williams na Chuo Kikuu cha Stanford vimeshikilia nambari mbili za juu, huku Chuo kinachoheshimika duniani Chuo Kikuu cha Harvard kikiwa nafasi ya saba ilhali mwaka jana kilishika nafasi ya nane.
Forbes waliweka orodha yao kwa kuzingatia vipengele vitano muhimu – kuridhika kwa mwanafunzi, mafanikio baada ya kuhitimu, deni la mwanafunzi, kiwango cha kufudhu, na mafanikio ya kitaaluma.
Orodha Vyuo na Vyuo Vikuu 10 bora Marekani.
1. Williams College
1. Williams College
2. Stanford University
3. Swarthmore College
4. Princeton University
5. Massachusetts Institute of Technology
6. Yale University
7. Harvard University
8. Pomona College
9. United States Military Academy
10. Amherst College
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni