Jumapili, 3 Agosti 2014
Bolt aibeba Jamaica
Bingwa wa mbio za mita 100 duniani Usain Bolt amelisadia taifa lake la Jamaica kufuzu katika fainali za 400 m x 100m hii leo licha ya tishio na kusisitiza kuwa amefurahi kuwa Glasgow.
Bolt amelazimika kukana madai kwamba alitoa matamshi mabaya dhidi ya mashindano hayo,
ambapo nusra jamaica ishindwe baada ya mmoja ya wakimbiaji wake katika mbio za 400m x 100m kupata jeraha.
Hatahivyo Bolt aliweza kuwasaidia wenzake na kushinda mbio hizo. Katika mahojiano yake na waandishi wa habari baada ya ushindi huo,
alisema kuwa alipatwa na wasiwasi juu ya mkasa huo lakini mwanariadha mwenzie wa Jamaica aliyeanza mbio hizo na kupata jeraha alimpokeza kijiti cha kukimbia hivyo kupelekea ushindi.
‘Kocha wangu kwa mara nyingi hutuambia tukimbie na uchungu’, alisema Bolt mwanadam mwenye kasi kubwa kuliko wote Duniani.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni