Jumamosi, 2 Agosti 2014
Kenyatta ataka ardhi kugawanywa upya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa agizo la kugawanywa upya kwa asilimia 70 ya ardhi ya Lamu ambapo kumekuwa na ghasia za vifo tangu mwezi Juni.
Alisema ukaguzi uliofanyika katika Kaunti ya Lamu ulionyesha kuwa waendelezaji 22 walijipatia ekari 500,000 ya ardhi ya serikali kinyume na utaratibu.
Hali ya hofu katika eneo hilo imechangia hasira dhidi ya watu wanaotoka maeneo mengine ya Kenya kujichukulia ardhi katika eneo la pwani.
Zaidi ya watu 100 wameuawa kwenye eneo la pwani kwa kuvamiwa na watu wenye silaha.
Kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Somalia la al-Shabab lenye uhusiano na al-Qaida limedai kuhusika na mashambulizi hayo, ila uongozi umewashukia kuhusika kwa wanamgambo wa nchini humo wenye mtandao wa kisiasa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni