Siasa ni jambo ambalo limeshikilia hatma ya vitu vingi sana duniani ikiwemo mchezo wa soka ambao una ufuasi mkubwa ulimwenguni kote.
Nchini Hispania – Raisi wa chama cha mpira wa miguu nchini Hispania (LFP) Javier Tebas amesema kwamba klabu ya FC Barcelona haitoweza kushiriki kwenye ligi ya nchi hiyo maarufu kama La Liga endapo tu kama jimbo la Catalunya lipata uhuru kutoka kwa Spain.
Jimbo la Catalunya ambalo lina miji minne ya Barcelona, Girona, Lleida, na Tarragona limekuwa likipigania uhuru wake kutoka Hispania kutokana na tofauti zao na nchi kwenye upane wa utamaduni na lugha.
FC Barca imekuwa alama ya harakati hizo za Catalunya lakini sasa Raisi wa LFP Javier Tebas amesema kwamba klabu iyo itashindwa kushiriki kwenye La Liga kwa sheria na kanuni zilizopo hivi sasa.
“Sipendi kufikiria suala hilo kutokea, naamini Catalunya itaendelea kuwa ndani ya Spain,” alikaririwa na gazeti la AS.
“Na sina pekee kwa FC Barcelona, pia vilabu Nastic, Girona, Espanol, Llagostera na Sabadell. Ikiwa sheria ya michezo itaendelea kubaki kama ilivyo, basi watashindwa kushiriki kwenye ligi yetu.”
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni