Ijumaa, 1 Agosti 2014
"CR7" Inamilikiwa kihalali na mtu mwingine sio Cristiano Ronaldo

Kuna uwezekano mkubwa Ronaldo akashindwa kuuza mavazi yake yenye lebo ya ‘CR7′ Marekani baada ya mtu mmoja nchini humo kufungua kesi dhidi ya mshambuliaji huyo wa Real Madrid kutokana na matumizi ya nembo ya “CR7″.
Christopher Renzi ambaye alilisajili jina la “CR7″ kibiashara (akiunganisha herufi za kwanza za majina yake na tarehe yake ya kuzaliwa: 7th October) nchini Marekani 2009 kwa matumizi ya website yake pamoja na label yake ndogo ya mavazi, aliandikiwa barua mara kadhaa na kampuni ya JBS Textile Group inayotengeneza bidhaa za ‘CR7′ za Cristiano Ronaldo, wakimwambia aache kutumia nembo hiyo.

Kwenye maongezi na shirika la habari la Marekani Reuters, mwanasheria wa Renzi alisema “Tunachohitaji na wao kutuacha huru bila usumbufu.”
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni