Sports and Entertainment

Ijumaa, 1 Agosti 2014

Magari bila dereva mbioni kuruhusiwa Uingereza

Hakuna maoni :

Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa itaziruhusu gari zisizokuwa na madereva barabarani ifikapo mwezi Januari mwakani.
Serikali hiyo pia imetoa wito miji ya Uingereza zitoe mapendekezo ya kuwania kuwa wenyeji wa moja kati ya majaribio 3 ya magari hayo.
Magari mapya yasiyo na dereva mbioni kuruhusiwa  kwenye barabara za Uingereza.
Magari mapya yasiyo na dereva mbioni kuruhusiwa kwenye barabara za Uingereza.
Aidha waziri huyo ameagiza kufanywe mabadiliko ya sheria za barabarani ilikuafikiana na mabadiliko hayo ya teknolojia.
Wizara ya usafiri wa umma nchini Uingereza ilikuwa imeahidi kuruhusu majaribio ya magari hayo mwisho wa mwaka uliopita.
Katibu wa Biashara Vince Cable aliyasema hayo katika hafla ya uzinduzi katika kiwanda cha kutengeneza magari cha Mira, kilichoko Midlands.
Waandisi nchini Uingereza wakishirikiana na wanavyuoni kutoka Chuo Kikuu cha Oxford wamekuwa wakifanya majaribio ya matumizi ya magari hayo yasiyo na madereva.
Wadau hata hivyo wamekuwa wakiibua tahadhari ya maswala ya Bima,na uhalali wa magari pasi na madereva jambo ambalo limewalazimu kutumia barabara za kibinafsi kwa majaribio yao.
‘Mimi mwenyewe nilijiskia kuwa salama ndani ya gari hilo lililokuwa bila dereva’ alisema bwana Cable.
Namna magari hayo yatakavyofanya kazi barabarani na kurahisisha huduma ya usafiri.
Namna magari hayo yatakavyofanya kazi barabarani na kurahisisha huduma ya usafiri.
Wakati huohuo Magari hayo yameruhusiwa kufanyiwa majaribio huko Marekani katika majimbo ya California, Nevada na Florida.
Gari linalotumiwa na kampuni ya mtandao wa Google tayari limetumika kwa zaidi ya kilomita laki tatu hivi katika mabarabara ya umma.
Mwaka uliopita kampuni ya 2013 ilifanya majaribio ya gari lake huko Japan.
Barani Europa kampuni ya kutengeza magari ya Volvo tayari imepata ithibati ya kujaribu magari yake mjini Gothenburg Sweden.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni