Ijumaa, 1 Agosti 2014
Ripoti ya matokeo ya vita kati ya Israel na Palestina
Zikiwa ni zaidi ya wiki tatu zimepita toka kuibuka tena kwa vita ya Israel dhidi ya Palestina, mpaka sasa utafiti unaonyesha ni zaidi ya watu 1450 wamepoteza maisha kutokana na mashambulizi.
Wanasema miongoni mwa waliofariki ni pamoja na zaidi ya Wananchi 800 wa Palestina, Wanajeshi 56 wa Israel lakini pia vilevile shule 130 zimebomolewa kwa mabomu.
Kingine ambacho ni hasara kubwa ni mabomu ya Israel yaliyobomoa nyumba/makazi zaidi ya elfu nne ambapo pia kwa upande mwingine Israel imelaumiwa kwa kusababisha mauaji ya ovyo na makusudi kwa kupoteza maisha kwa wasio na hatia wakiwemo watoto ambao walikua wamejihifadhi na wazazi wao kwenye shule zinazomilikiwa na Umoja wa mataifa ambazo pia zilishambuliwa.
Wapalestina hawa walilazimika kujihifadhi kwenye shule za umoja wa mataifa baada ya makazi yao kushambuliwa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni