Jumamosi, 2 Agosti 2014
Ronaldo aikwepa Man U huko Marekani
Mchezaji bora wa Dunia kwa mwaka 2014 Cristiano Ronaldo 29 anayecheza klabu ya Real Madrid anatazamiwa kulikosa pambano la kirafiki dhidi ya timu yake ya zamani klabu ya Man-U.
Habari kutoka kwa kocha Carlo Ancelotti zimethibitisha kutokuepo kwa staa huyo kutokana na kutokuwa fiti kwa 100% , ikumbukwe Ronaldo alikuwa akisumbuliwa na majeraha tangu mechi za mwishoni mwaligi msimu uliopita,
kitu kilichopelekea kutokung’aa katika michuano iliyopita ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Brazil.
Ronaldo alijiunga na kikosi cha Los blancos kilichopo Marekani akitoke mapumzikoni tarehe 26 ya mwezi Agosti lakini hakuweza kufanya mazoezi ya pamoja na kikosi cha kwanza ilikujiweka fiti na mchezo wa leo Jumamosi.
Hatahivyo kocha Carlo Ancelotti amesisitiza kuwa hivisasa staa huyo ameandaliwa ratiba maalumu kwaajili ya kujiweka sawa kabla ya msimu mpya kuanza
na wamepanga kumtumia katika mechi ya Supercopa mara baada ya kurudi Hispania.
Kwahiyo ilo ‘game’ dhidi ya vijana wa Van Gaal atalishuhudia akiwa jukwaani, na muda wa mechi hiyo ni saa tano usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni