Sports and Entertainment

Alhamisi, 18 Septemba 2014

Wananchi mkoa wa Kigoma wamevitaka vyombo vya dola nchini kuboresha mafunzo ya kijeshi.

Hakuna maoni :
Wananchi katika mkoa wa Kigoma, wamevitaka vyombo vya dola hapa nchini kuboresha mafunzo ya kijeshi katika ngazi mbalimbali kulingana na kuongezeka kwa kasi ya uhalifu duniani, matumizi ya silaha na mbinu mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumiwa kuangamiza  watu wasio na hatia.


Wakizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya jeshi la kujenga taifa oparesheni miaka hamsini kwa vijana kwa mujibu wa sheria katika kambi ya bulombora wilayani uvinza wamesema jeshi linapaswa kuendelea kujizatiti dhidi ya maadui wa taifa huku wahitimu wakieleza kuwa katika mafunzo hayo kwa vijana waliomaliza kidato cha sita wamejifunza mambo ambayo yamewajenga na kuwasaidia kujitambua.
 

Akihutubia baada ya kukagua gwaride la kufunga mafunzo hayo, mkuu wa mkoa wa kigoma Luten kanal mstaafu Issa Machibya amewataka wahitimu hao kuyatumia mafunzo waliyoyapata kwa manufaa yao na taifa na kutanguliza uzalendo katika utumishi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni