Sports and Entertainment

Alhamisi, 18 Septemba 2014

Pardew Kukabidhi Mikoba Kwa Mchezaji Wake Endapo Atazikosa Point 3 Za Hull City

Hakuna maoni :

Beki kutoka nchini Argentina Fabricio Coloccini ametajwa kwenye orodha ya watu wanaotarajiwa kuirithi nafasi ya ukuu wa benchi la ufundi la klabu ya Newcastle Utd, endapo Alan Scot Pardew atashindwa kufaulu mtihani wa kuibuka na ushindi mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Hull City.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la Telegraph zimeelza kwamba, Coloccini ambaye kwa sasa ni beki wa kutumainiwa wa kikosi cha Newcastle Utd ameingizwa kwenye orodha hiyo kutoka na umakini ambao kila leo amekua akiuonyesha dhidi ya wachezaji wengine klabuni hapo.
Gazeti hilo limeendelea kueleza kuwa mmiliki wa klabu ya Newcastle Utd Mike Ashley anafikiria kufanya maamuzi hayo ya kushangaza kutokana uchunguzi alioufanya na kubaini beki huyo ambaye pia ni nahodha wa kikosi cha The Magpies amekuwa na mahusiano ya karibu na wachezaji wenzake hivyo hali hiyo inaaminika huenda ikaleta utulivu.
Sababu nyingine iliyotajwa kwenye gazeti hilo ya kutaka kuteuliwa kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 32, ni kutaka kuepuka gharama kubwa ambazo huenda zikaifanya klabu ya Newcastle Utd kushindwa kumpata meneja mzuri katika kipindi hiki ambacho wanahangaikia suala la kusaka matokeo mazuri kutokana na kuanza vibaya msimu.
Wengine walionekana kwenye orodha ya kutaka kumrithi Alan Pardew ni meneja wa sasa wa klabu ya Hull City Steve Bruce pamoja na David Moyes ambaye hana kibarua baada ya kuonyeshwa malango wa kutokea Old Trafford mwanzoni mwa mwaka huu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni