Alhamisi, 18 Septemba 2014
WENGER : najuta kutomsajili Ronaldo
kocha wa washika bunduki wa jiji la London Arsenal, Arsenal Wenger ametoboa siri ya kwamba katika usajili anaojutia ni ule wa kumkosa Mchezaji nguli wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo
Ronaldo , ambaye hadi sasa ameshatwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia mara mbili moja katika klabu zote mbili alizochezea akianzia makali yake Old Traford mwaka 2008 kabla ya kufanya hivyo tena mwaka 2013
Mreno huyo ambae pia kwa miaka ya 2006 hadi 2009 ameiwezesha manchester kushinda taji la ligi kuu Uingereza misimu ambayo Wenger aliambulia mikono mitupu
"Najuta, nilikaribia kabisa kumsajili Cristiano Ronaldo" alijibu wenger katika kipindi cha maswali na majibu cha Huawei
"Na tena sio kwamba sikumsajili bali alienda Manchester United , hii inauma hadi leo"
Wenger pia amedai kuwa angependa sana mchezaji nguli wa Chelsea Didier Drogba angekuwa katika himaya yake lakini hatimae mchezaji huyo alitua darajani
"Ningependa kuwa na Drogba kwa misimu miwili"
"nilimkosa wakati alipokua Ufaransa, nilijua kabisa kuna mchezaji mzuri kule , haikua ligi kubwa lakini nilimkosa"
"Mbaya sana anafunga sana katika mechi kubwa"
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni